Sunday, 4 January 2015
MSHTUKO: KIFO CHA MTOTO WA RAILA ODINGA
Fidel Odinga, mtoto mkubwa wa kiume wa kiongozi wa chama cha Cord cha Kenya, Raila Odinga, alikutwa siku ya Jumapili asubuhi nyumbani kwake Windy Ridge, Karen baada ya kurejea usiku alipotoka na rafiki zake.
Mwili wa mtoto huyo wa Raila ulikutwa kitandani. Polisi walisema mpaka sasa haijajulikana chanzo cha kifo chake.
Aliyezaliwa mwaka 1973, marehemu Fidel alimwoa mwanamke kutoa Eritrea, Getachew Bekele,ambaye amezaa naye mtoto mmoja.
Fidel alikuwa mtoto mkubwa katika familia ya watoto wanne Rosemary, Raila Junior na Winnie.
Taarifa ya kifo chake tu kilipojulikana, ujumbe wa kutoa pole ulimiminika kwenye mitandao ya kijamii.
Kurasa za Facebook zikafunguliwa na kusababisha wafuasi wengi kuzifuata saa chache baada ya kifo chake.
Chanzo: nation.co.ke
Imetafsiriwa na mwandishi wetu
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment