Saturday, 10 January 2015

MUUGUZI AUA WAGONJWA 30 KISA 'KUBOREKA'



 


Mahakama ya Ujerumani imeambiwa aliyekuwa muuguzi wa kiume amekiri kuua zaidi ya wagongwa 30 kwenye hospitali alipokuwa akifanyia kazi, kwa madai kuwa ‘kaboreka tu’.

Mtaalamu wa magonjwa ya akili alisema wakati wa kesi hiyo kuwa muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 38 alikiri kufanya mauaji hayo katika uchunguzi aliofanyiwa hivi karibuni, msemaji wa mahakama alisema.

Kesi ya aliyekuwa muuguzi huyo ilianza Oldenburg,  kaskazini mwa Ujerumani mwezi Septemba, akituhumiwa kwa mauaji ya wagonjwa watatu na jaribio la mauaji ya wengine wawili.

Mtaalamu huyo alisema alikiri mashtaka hayo, na pia akasema alizidisha kipimo cha dawa kwa wagonjwa wengine 90, ambapo 30 walifariki dunia, msemaji huyo alisema.


Wachunguzi wanahisi nia yake ilikuwa kuibua dharura za kitabibu ili apate nafasi ya kuonyesha ujuzi wake wa kumwibua mgonjwa aliyezimia, lakini pia alikuwa ‘ameboreka tu’.

Inaaminiwa alikuwa akiwachoma wagonjwa na sindano yenye dawa ya kutibu moyo iliyovuruga mapigo ya moyo na kushusha kiwango cha damu.

Chanzo: AP






No comments:

Post a Comment