Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia amepata maradhi ya mapafu
'Pneumonia'na amekuwa akipumua kwa kutumia mrija, maafisa wa nchi hiyo walisema.
Mfalme huyo, anayeaminiwa kuwa na umri wa miaka 90, alilazwa hospitalini siku ya Jumatano kwa uangalizi.
Mfalme Abdullah, aliyeshika nafasi hiyo kuanzia mwaka 2005, amekuwa akiumwa mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.
Umri wake na afya yake umefanya wengi kujiuliza kuhusu urithi wa ufalme nchini humo.
Crown Prince Salman, mwenye umri wa miaka ya 70, ndiye anayefuata kwenye urithi wa ufalme, japo bado kuna maswali kuwa nani atachukua nafasi hiyo.
Ufalme huo umepita kwa watoto wa kiume wa muasisi na baba wa taifa wa Saudi Arabia Ibn Saud, lakini wachache sana bado wako hai.
Mwaka jana, Mfalme Abdullah alichukua hatua ya kuteua naibu, ambaye ni mdogo wake wa baba mmoja Prince Muqrin, kwa nia ya kujaribu kuweka hali ya kuwepo hali tulivu ya kurithishana.
Chanzo: AFP
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment