Wednesday, 7 January 2015

MUHAMMAD ALI ATOLEWA HOSPITALI


Muhammad Ali
Picha imepigwa 2006

Bondia wa mabondia Muhammad Ali ametolewa hospitalini baada ya kulazwa mwezi uliopita alipopatwa na maambukizi katika njia ya mkojo.

Aliyekuwa bingwa mara tatu wa uzani wa juu wa masumbwi duniani, amerejea nyumbani baada ya kutolewa siku ya Jumanne, msemaji wa familia alisema.

Bob Gunnell alisema Ali mwenye umri wa miaka 72 amepona kabisa na familia yake inamshukuru kila mmoja kwa sala zao.

Ali alitambuliwa kuwa na ugonjwa wa kutetemeka ‘Parkinsons’ mwaka 1984 baada ya kustaafu ndondi.

Alionekana hadharani mwezi Septemba, eneo alipokuzwa Louisville katika sherehe za kutoa  Tuzo za Kutetea Haki za Binadamu za Muhammad Ali.

Jina la hospitali ambapo Ali alitibiwa halijatolewa.

Chanzo:AP

No comments:

Post a Comment