Sunday, 4 January 2015

MSHUKIWA WA SHAMBULIO LA TZ NA KENYA AFARIKI



Anas Al-Liby shown in FBI photo
Anas al-Liby alikana kuhusika na ugaidi Marekani

Anayedaiwa kuwa kiongozi wa al-Qaeda amefariki dunia siku chache tu kabla ya kufikishwa mahakamani mjini New York kutokana na mashambulio ya mwaka 1998 barani Afrika kwenye mabalozi ya Marekani.

Abu Anas al-Liby, mwenye umri wa miaka 50, alikufa hospitalini siku ya Ijumaa, mke wake na wakili wake walisema.

Inaripotiwa alikuwa na saratani ya ini.

Bw Liby alikamatwa kwenye uvamizi uliofanywa na Marekani mjini Tripoli Oktoba 2013.

Alitakiwa kufikishwa mahakamani Januari 12 kutokana na mashambulio ya ubalozi mwaka 1998, yalioua zaidi ya watu 220 nchini Kenya na Tanzania.

Bw Liby, ambaye jina lake la ukweli ni Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, awali alikana mashtaka ya kuhusishwa na ugaidi.

Mke wake, Um Abdullah, aliishutumu serikali ya Marekani siku ya Jumamosi kwa “kumteka, kumfanyia mabaya na kumwuua mtu asiye na hatia,” kulingana na shirika la habari la AP.

No comments:

Post a Comment