Thursday 15 January 2015

CHARLIE HEBDO: MAGAZETI YA AFRIKA YAOMBA RADHI


Apology published by Kenya's The Star on 15 January 2015
Gazeti la The Star lina ushawishi Kenya

Magazeti mawili ya Afrika yameomba radhi kwa kuchapisha ukurasa wa juu wa jarida la  Charlie Hebdo likiwa na kibonzo cha Mtume Muhammad, baada ya wasomaji wa Kiislamu kulalamika.

Gazeti la Kenya The Star na The Citizen la Afrika kusini yamesema yanajuta kwa kuwakosea Waislamu.  

Chombo cha kudhibiti vyombo vya habari Kenya kimemwita shaurini mmiliki wa gazeti la Star baada ya kulishutumu kukiuka sheria ya kuheshimiana.

Nchini Senegal, serikali imepiga marufuku usambazaji wa jarida hilo la Charlie Hebdo.

Gazeti la pili la Kenya, Business Daily, nalo limechapisha ukurasa huo wa mbele wa jarida hilo la Ufaransa.

Katika toleo lake la Alhamis asubuhi, The Star lilisema wasomaji wengi wa Kiislamu wamelalamika juu ya “uzalishaji mdogo” wa ukurasa wa mbele wa Charlie Hebdo siku ya Jumatano.  

Wakiomba radhi, gazeti hilo, la tatu kwa ukubwa Kenya, limesema “linajuta sana kwa kosa na uchungu uliosababishwa na picha hiyo”.

No comments:

Post a Comment