Wednesday 11 February 2015

WASHINDI IVORY COAST WAMWAGIWA FEDHA


Ivorian President Alassane Ouattara and Ivory Coast captain Yaya Toure wave at the crowd

Timu ya mpira ya Ivory Coast imezawadiwa mamilioni ya dola na serikali ya nchi hiyo kwa kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika.

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara anampa kila mchezaji ambao jumla wako 23, nyumba yenye thamani ya dola 52,000 kila moja na pia pesa taslimu ya kiwango hicho hicho kwa kila mmoja, serikali hiyo ilisema.

Timu hiyo imeishinda Black Stars ya Ghana 9-8 kwa mikwaju wa penalti kwenye fainali ya shindano hilo Equatorial Guinea.

Shirikisho la Soka la nchi hiyo pia limepewa mamilioni ya fedha na wafanyakazi wengine wa timu hiyo.

Kwa jumla serikali hiyo imetoa zaidi ya dola milioni 3 kwa kusherehekea ushindi huo.
Timu ya Ghana nao hawakuachwa nyuma, licha ya kushindwa.

Kila mchezaji amepewa dola 25,000 na mfadhili wa timu hiyo, ambao ni shirika la mafuta la taifa Ghana (GNPC), kiwango ambacho waziri wa michezo wa Ghana ameona ni kidogo.


No comments:

Post a Comment