Monday, 23 February 2015

KESI YA BI GBAGBO WA IVORY COAST YAANZA



 Ivory Coast"s former first lady Simone Gbagbo waves as she arrives at the Court of Justice in Abidjan, on February 23, 2015

Aliyekuwa mke wa rais wa Ivory Coast, Simone Gbagbo, amekana kuwa na kosa lolote katika madai ya kuhusika kwenye ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Bi Gbagbo alikuwa akitoa ushahidi kwa mara ya kwanza katika kesi yake huko Abidjan.

Mume wake, ambaye alikuwa rais Laurent Gbagbo, anasubiri kesi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Alikataa kukubali kuwa alishindwa katika uchaguzi wa rais, yaliyochochea ghasia kwa miezi kadhaa yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000.

Pia alisistiza mume wake alikuwa mshindi halali wa uchaguzi badala ya mpinzani wake, Alassane Ouattara, aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi huo.

Polisi walipata kazi ya kuwatenganisha wafuasi na wapinzani wa Gbagbo baada ya mfarakano ulipoibuka nje ya mahakama.

No comments:

Post a Comment