Sunday, 8 February 2015

UCHAGUZI WA MWEZI HUU NIGERIA WAAHIRISHWA



People hold signs to protest against the postponement of elections, in Abuja, Nigeria, 7 February 2015
Mapema Jumamosi, waandamanaji wengi wametoa wito wa uchaguzi kuendelea kama ilivyopangwa

Upinzani wa Nigeria umesema hatua ya kuahirisha uchaguzi wa rais wa Februari 14 kwa wiki sita “una athari kubwa kwa demokrasia”.

Tume ya uchaguzi imesema imesogeza tarehe ya upigaji kura kwasababu majeshi yaliyotakiwa kufanya ulinzi kwenye vituo vya kupigia kura yamesambazwa kupambana na Boko Haram

Kuahirishwa kwa uchaguzi huo kumeifurahisha chama tawala, lakini Marekani imesema “imesikitishwa”

Nigeria imekuwa ikipambana na wapiganaji wa Boko Haram kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.

Maelfu ya watu wamekufa kutokana na mapigano ya wapiganaji hao katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Boko Haram pia imeanza kushambulia majirani wa Nigeria: siku ya Jumapili, kwa mara ya pili katika siku tatu, wapiganaji hao wameshambulia mji wa Diffa mpakani mwa Niger.

Takriban mtu mmoja alifariki dunia kwenye mlipuko katika soko la mji huo, huku baadhi ya walioshuhudia wakisema mtu aliyejitoa mhanga ndiye kahusika.

No comments:

Post a Comment