Friday, 6 February 2015

MWANAMKE AKAMATWA LONDON KWA 'UKEKETAJI'



Border control at Heathrow Airport

Mwanamke mmoja amekamatwa uwanja wa ndege wa Heathrow kwa kosa la njama ya kufanya ukeketaji.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa ndio kwanza ana mpango wa kupanda ndege iliyokuwa ikielekea Ghana kupitia Amsterdam alipokamatwa na maafisa waliokuwa wakifanya harakati za kuelimisha watu kuhusu ukeketaji.

Raia huyo wa Uingereza aliyezaliwa Zimbabwe, alipelekwa kituo cha polisi magharibi mwa London.

Binti mwenye umri wa miaka minane aliyefuatana na mwanamke huyo alipelekwa ustawi wa jamii.

Polisi walifanya harakati hizo uwanja wa ndege kutoa elimu sambamba na siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji.

No comments:

Post a Comment