Wednesday, 4 February 2015

WAPIGANAJI WAWILI WANYONGWA JORDAN



Sajida al-Rishawi in military court in Jordan. Photo: 2006
 Sajida al-Rishawi alipewa hukumu ya kifo huko Jordan kwa takriban muongo mmoja 

Jordan imewanyonga wafungwa wawili, akiwemo mpiganaji mmoja wa kike, kufuatia mauaji ya rubani wao mmoja wa kijeshi aliyeuawa na wapiganaji wa Islamic State (IS).

Mwanamke huyo, aliyekuwa amejitolea mhanga lakini hakufanikiwa Sajida al-Rishawi, na mshirika wa al-Qaeda Ziyad Karboli – wote wakiwa raia wa Iraq – walinyongwa alfajiri, maafisa walisema.

Mauji hayo kwa kunyonga yalifanyika saa chache baada ya IS kuweka video ikionyesha rubani Moaz al-Kasasbeh akichomwa moto ilhali yuko hai.

Alikamtwa baada ya kupata ajali wakati wa kupambana na IS huko Syria mwezi Desemba.

Jordan ilikuwa ikifanya jaribio la kumwokoa Lt Kasasbeh ili aachiwe huru kwa kubadilishana naye na Rishawi.

Rishawi alipewa hukumu ya kifo kwa kuhusika na mashambulio katika mji mkuu wa Jordan, Amman, ulioua watu 60 mwaka 2005.

Karboli alitiwa hatiani mwaka 2008 kwa kumwuua raia wa Jordan.

No comments:

Post a Comment