Tuesday, 3 February 2015

BOBBI KRISTINA BROWN 'HALI MAHUTUTI'



Whitney Houston (left) and daughter Bobbi Kristina Brown. Photo: 2011
Whitney Houston pamoja na Kristina Brown mwaka 2011

Bobbi Kristina Brown, binti wa mwimbaji marehemu Whitney Houston, "yuko katika hali mbaya” baada ya kukutwa hana fahamu, familia yake imesema.

Bi Brown, mwenye umri wa miaka 21, alikimbizwa hospitalini siku ya Jumamosi baada ya kukutwa katika hali hiyo ya kupoteza fahamu bafuni nyumbani kwake mjini Atlanta.

Mama yake, aliyekuwa aking’ara duniani kote, alikutwa amefariki dunia Februari 2012, akiwa na umri wa miaka 48, bafuni katika hoteli Los Angeles.

Hospitali haijsema lolote kuhusu hali yake ila familia yake imesema wapo naye.

Taarifa iliyotolewa, na familia ya Bi Brown: "Bobbi Kristina anapambana na amezungukwa na familia yake."

"Tunawaomba mheshimu ombi letu la kutuachia faragha wakati huu mgumu."

Siku ya Jumatatu, polisi walisema waliitwa nyumbani kwake Atlanta siku ya Jumamosi kwa minajil ya mtu “kuzama”.

Afisa mmoja wa polisi aliiambia redio moja kuwa hawakukuta dawa zozote za kulevya nyumbani kwake.

Baba yake Bobbi Kristina ni msanii maarufu wa miondoko ya hip-hop Bobby Brown.

No comments:

Post a Comment