Tuesday, 10 February 2015

KANYE WEST ASEMA GRAMMYS 'HAZIHESHIMU SANAA'





Kanye West ameshutumu tuzo za Grammys kwa "kutoheshimu sanaa" baada ya kumpa ushindi Beck wa albamu bora ya mwaka badala ya Beyonce.

Alikuwa almanusra kuvamia jukwaa wakati Beck alipokuwa akitoa hotuba yake ya shukran.

Ilionekana kama West alikuwa arudie tukio alilofanya dhidi ya Taylor Swift, alipovamia jukwaa mwaka 2009.

Hatahivyo, alipohojiwa kwenye kipindi cha E, baadae alisema aliamua kutabasamu na kukaa chini baada ya kumfikiria binti yake.

 Msanii huyo wa miondoko ya hiphop alisema anaona Beck “angetakiwa kumpa Beyonce tuzo yake”.

"Ninachojua ni kuwa hizi tuzo za Grammys, kama wanataka wasanii wa kweli wawe wanarejea, wanatakiwa kuacha kutuchezea akili. Hatutoendelea kuzinguliwa nao." Alikiambia kipindi cha E, alipohojiwa akiwa na mkewe Kim Kardashian.

No comments:

Post a Comment