Friday 24 October 2014

MGONJWA WA KWANZA WA EBOLA APATIKANA MALI



 Health worker in Mali. Photo: 9 October 2014

Serikali ya Mali imethibitisha kuwepo mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini humo. 

Inasemwa kuwa mtoto wa kike wa miaka miwili amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huo. Hivi karibuni alirejea kutoka Guinea.

Zaidi ya watu 4,800 wamefariki dunia kutokana na Ebola – hasa Liberia, Guinea na Sierra Leone – tangu mwezi Machi.

Wakati huo huo, timu ya wanasayansi imeundwa kutathmini uwezo wa kutumia damu ya wagonjwa waliopona baada ya kuugua Ebola na itumike kama tiba.

Matumaini ni kuwa kinga za asili za mwili ‘antibodies’ zinazotumiwa na mfumo wa kinga mwilini kupambana na Ebola zinaweza kuhamishwa kutoka aliyepona hadi kwa mgonjwa.Utafiti huo utaanzia Guinea.

Vile vile, daktari mmoja kutoka New York aliyerejea hivi karibuni kutoka nchini Guinea ambapo wengi wameathirika na ugonjwa huo amekutwa ana virusi vya Ebola.

Dr Craig Spencer, aliyewatibu wagonjwa waliokuwa na Ebola wakati akifanya kazi na shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medecins Sans Frontieres (MSF), kuanza kupata homa siku ya Alhamis, siku chache aliporejea.

Ni wa kwanza kugunduliwa na Ebola mjini New York, na mgonjwa wa nne Marekani kukutwa na virusi hivyo.

No comments:

Post a Comment