Msemaji wa kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas ameelezea kufungwa kwa eneo lenye utata la sehemu takatifu la Jerusalem ni “kutangaza vita”.
Hatua hii imekuja baada ya kuwepo mvutano na vurugu kufuatia kupigwa risasi kwa mwanaharakati wa Kiyahudi.
Waziri mkuu wa Israel ametoa wito wa kuwepo utulivu, akisema Bw Abbas anachochea ghasia.
Eneo hilo takatifu litafunguliwa tena Ijumaa, waziri wa uchumi wa Israel alisema.
Yehuda Glick, mwanaharakati wa Wayahudi alijeruhiwa.
Polisi wa Israel baadae walimwuua Mpalestina anayeshukiwa kumpiga risasi mwanaharakati huyo.
Moataz Hejazi, mwenye umri wa miaka 32, alipigwa risasi baada ya kufyatua risasi alipokuta amezingirwa na polisi nyumbani kwake.
Rabbi Glick ni mwanaharakati maarufu, mzaliwa wa Marekani anayeteta haki za Wayahudi kufanya ibada kwenye eneo hilo, ambapo kwa sasa huzuiliwa.
Jengo hilo – linalojulikana kwa Wayahudi kama Temple Mount na Waislamu wanapaita Haram al-Sharif –, ni sehemu takatifu kwa Wayahudi na pia una msikiti wa al-Aqsa - eneo takatifu la tatu katika Uislamu.
Katika taarifa nyingine
- Sweden imekuwa nchi ya kwanza kubwa upande wa Ulaya kuitambua rasmi Palestina kama taifa – Israel imemrejesha balozi wake wa Sweden kutokana na hilo, kulingana na afisa mmoja aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP.
- Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeisihi Israel kusimamisha ujenzi wao wa makazi kwenye ukanda wa Gaza na kuchunguza madai ya ukiukwaji wa sheria unaofanywa na majeshi yake huko Gaza tangu mwaka 2008.
- Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alielezea madai ya kutolewa matusi na afisa mwandamizi kutoka Marekani dhidi ya Bw Netanyahu ni jambo la “aibu, lisilokubalika na lenye madhara”
Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
No comments:
Post a Comment