Friday, 24 October 2014

WA KWANZA KUPATA EBOLA MALI AFARIKI DUNIA



A woman's temperature is checked at the Guinea-Mali border, 2 October 2014
Watu kutoka Guinea wanapimwa joto la mwili kabla ya kuingia Mali

Maafisa wa afya wanahofia watu wengi walimgusa muathirika wa kwanza wa Ebola kutoka Mali – mtoto wa miaka miwili.

Hivi karibuni aliwasili Guinea, miongoni mwa nchi zilioathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa huo, na amefariki dunia.

Mtoto huyo alionyesha dalili, zikiwemo kutoka damu puani, wakati akisafiri kwenye basi la umma na kupita miji mbalimbali, lilisema shirika la Afya Duniani (WHO).
 
Watu 43, wakiwemo wafanyakazi wa afya10, ambao walimgusa kwa namna moja au nyingine wametambuliwa na kutengwa.

Mama wa mtoto huyo alifariki dunia nchini Guinea wiki chache zilizopita ambapo ndugu zake wakamchukua mtoto na kwenda naye Mali.

Zaidi ya watu 4,800 wamefariki dunia kutokana na Ebola – hasa Liberia, Guinea na Sierra Leone – tangu mwezi Machi.

No comments:

Post a Comment