Friday, 31 October 2014

RAIS WA BURKINA FASO AJIUZULU





Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore ametangaza kujiuzulu, kufuatia maandamano yenye ghasia katika jaribio lake la kuongeza uongozi wake wa miaka 27.

 Bw Compaore alitoa taarifa akisema nafasi ya rais sasa iko wazi.

Msemaji wa jeshi naye aliwaeleza waandamanaji walioshangilia sana katika mji mkuu, Ouagadougou.

Awali, waandamanaji walikasirishwa na nia yake hiyo, hivyo kuchoma moto bunge na majengo ya serikali.

Bw Compaore alisema atakabidhi madaraka baada ya serikali ya mpito kukamilisha muda wake wa miezi 12.

Katika tangazo lake la awali, Bw Compaore alitoa wito wa jeshi kutekeleza hatua za dharura za kuzingira maeneo yenye maandamano hayo.


A man stands in front of a burning car, near the Burkina Faso's Parliament where demonstrators set fire to parked cars - 30 October 2014, Ouagadougou, Burkina Faso
Waandamanaji walichoma moto magara, jengo la bunge na majengo ya serikali

Hatua hiyo ilifuatiwa na mkutano wa waandishi wa habari ambapo mkuu wa jeshi Jenerali Honore Traore alitangaza “chombo cha mpito kitaundwa kwa ushirikiano wa vyama vyote”.

Ujumbe maalum wa katikbu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wa Afrika magharibi, Mohamed Ibn Chambas, ataelekea Burkina Faso siku ya Ijumaa katika jitihada za kutuliza mgogoro huo.

Nia yake ya kugombea tena urais ulichochea maandamano kwenye mji mkuu Ouagadougou. Maandamano hayo ni ya hatari kutokea dhidi ya uongozi wa Bw Compaore.

  • Alihudumu chini ya Rais Thomas Sankara kama waziri kiongozi
  • Alichukua madaraka baada ya Sankara kuuawa katika mazingira ya kutatanisha na kundi la askari mwaka 1987
  • Rais wa kwanza wa kuchaguliwa mwaka 1991 na 1998
  • Katiba mpya ya mwaka 2000 inatoa nafasi ya mihula miwili tu madarakani, na miaka mitano kila muhula.
  • Akashinda mihula mengine miwili ya ziada
  • Maandamano ya kupinga jaribio la kubadili muda wa mihula hiyo ilianza mwaka mmoja uliopita, ikichochewa na gharama kubwa za maisha.

No comments:

Post a Comment