Saturday 25 October 2014

GIBNEY, AFUMWA KUOA MKE WA PILI FACEBOOK



Maurice Gibney
Maurice Gibney, Yvonne Gibney (juu kulia) na Suzanne Prudhoe (chini kushoto)

Kama wanandoa wengine wote, Yvonne na Maurice Gibney walikuwa na misukosuko kwenye ndoa yao.

Aliwahi kusoma kuhusu tetesi za uwezekano wa mumewe kutoka nje ya ndoa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, lakini akawa na imani kuwa ilikuwa ni uzushi tu na hawezi kumwendea kinyume wakati alipokuwa akifanya kazi Oman.

Wazo hilo lilibaki mpaka alipogundua picha ya mume wake huyo mwenye watoto wawili  akiwa anamwoa mwanamke mwengine kwenye ufukwe wa bahari katika taifa hilo la Kiarabu.

Bila kujua Bi Gibney, mwenye umri wa miaka 55, mumewe anayefanya kazi kwenye kampuni ya mafuta amekuwa akiishi maisha mengine na mwalimu Suzanne Prudhoe, mwenye umri wa miaka 46.

Baadae ilikuja kujulikana wawili hao walikuwa wapenzi kwa takriban miezi 18 kabla ya kufanya sherehe baharini yenye kugharimu £45,000 kwenye ubalozi wa Uingereza, mwezi Machi mwaka jana.

 Baada ya kukasirishwa sana kwa kuendewa kinyume, Bi Gibney, mhudumu wa afya, akageuka kuwa mchunguzi na kugundua mumewe alimdanganya mpaka mama yake mwenyewe, ambaye alihudhuria harusi hiyo ya pili pamoja na mtoto wa kambo, ili kuwashawishi kwamba tayari walishatalakiana.

Bi Gibney alizungumzia ‘uchungu’ alioupata baada ya mume huyo walioachana, ambaye ana kipato cha paundi 85,000 kwa mwaka bila kukatwa kodi, alipoondoka mahakamani baada ya kukiri kuwa na wake wawili. Badala ya kumfunga jela jaji amemtoza faini ya paundi 85.

 ‘Wakati akioa mke mwengine tulikuwa tumeoana miaka 17,’ alisema. ‘Niliithamini ndoa yangu na nilimpa heshima, imani, mapenzi na kila kitu.

Mahakamani ilijulikana kuwa Bi Gibney aligundua kuhusu siri hiyo nzito Februari mwaka jana.

Baada ya kuona watu wakitoa maoni yao Facebook, alishtuka  alipobonyeza ukurasa wa Bi Prudhoe na kukuta picha za mumewe, mwenye umri wa miaka 49, aliyevaa suti ya rangi ya maziwa, akimbusu na kumtazama machoni kwa mahaba mke wake mpya.


Chanzo: Dailymail.co.uk


Imetafsiriwa na Mwandishi wetu


 

No comments:

Post a Comment