Friday 31 October 2014

MAUAJI YA KUTISHA DRC





Mkusanyiko wa watu ulimpiga mawe mpaka kumwuua kijana mmoja wa kiume kaskazini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Ijumaa kabla ya kumchoma moto na kula maiti yake.

Mashahidi wanasema, ilikuwa ni kisasi baada ya kuwepo mfululizo wa mashambulio yaliyofanywa na waasi wa Uganda.

Tukio hilo lililotokea mjini Beni lilifuatiwa na uvamizi usiku katika eneo hilo huku wakilaumiwa kundi la ADF-NAUL, wanaodhaniwa kuwaua zaidi ya watu 100 mwezi huu, wakitumia mapanga.

Walioshuhudia walisema mtu huyo, ambaye hajatambuliwa mpaka sasa, alizua wasiwasi ndani ya basi baada ya abiria kugundua hakuweza kuzungumza lugha ya Kiswahili na alikuwa amebeba panga.

Akizungumza mjini Beni, Rais wa Congo Joseph Kabila alisema khatima ya wapiganaji wa ADF-NALU itakuwa kama ile iliyowakumba kundi la M23, lililomalizwa na jeshi linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa mwaka jana.

Chanzo: news.yahoo.com       
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu

No comments:

Post a Comment