Friday, 31 October 2014
MTANGAZAJI MAARUFU TZ, BEN KIKO AFARIKI DUNIA
Mtangazaji maarufu wa zamani wa redio Tanzania (TBC) Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Oktoba 31 katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili jijini Dar alikokuwa akipatiwa matibabu.
Ben Kiko ambaye jina lake kamili ni Ben Hamisi Kikoromo alihamishiwa katika hospitali ya jeshi ya Milambo, mkoani Tabora ambapo alilazwa kwa ajili ya matibabu ya figo kwa muda wa wiki mbili.
Mzee Kiko alijizolea umaarufu katika tasnia ya utangazaji wakati wa vita ya Kagera (Tanzania na Uganda-1979) kutokana na taarifa zake za kusisimua wakati wa mapigano hayo.
Mwaka 2012 mwanahabari huyo mkongwe alitunukiwa tuzo ya fanaka ya maisha (Lifetime Achievement Award) kutokana na mchango wake katika uandishi wa habari.
Kabla mauti hayajamfika Ben Kiko alikuwa akifanya kazi katika redio ya Voice of Tabora inayomilikiwa na Mbunge wa Tabora Mjini Ismail Aden Rage.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin.
Chanzo: taarifa.co.tz / michuzi blog
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment