Friday, 12 December 2014
PHARRELL WILLIAMS AZOA TUZO ZA MUZIKI ZA BBC
Pharrell Williams amekuwa king’ara katika tuzo za kwanza za kipekee za muziki za BBC.
Mtayarishaji na mwandishi wa muziki huyo kutoka Marekani alitajwa kuwa msanii bora wa kimataifa na kushinda nyimbo bora ya mwaka kwa kibao chake cha Happy.
Ed Sheeran alitajwa kuwa msanii bora wa mwaka wa Uingereza, na pia aliimba wimbo wake bomba kabisa uliotengenezwa na Pharerell, uitwao Sing, akitumia tu gitaa lake.
Shughuli hiyo pia ilishuhudia wasanii One Direction, Take That na Coldplay wakiimba jukwaani.
Pharrell alishindwa kuhudhuria tuzo hizo, kwani alikuwa akirekodi onyesho la vipaji la Marekani liitwalo The Voice.
Aliunganishwa na sherehe hizo kwa njia ya satelaiti, na kuelezea mafanikio ya kibao hicho cha Happy kuwa ni cha “ajabu” na “si jambo analoweza kuelezea yeye mwenyewe”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment