Wednesday, 10 December 2014

KENYA YACHUNGUZA RIPOTI YA AL-JAZEERA

Taarifa ilituhumu kuwa mpiganaji wa Kiislamu aliuawa na polisi nje ya msikiti mjini Mombasa.

Kenya imetoa agizo la kuchunguza kituo cha Al-Jazeera na kukifungulia mashtaka kutokana na ripoti za kutuhumu polisi wa nchi hiyo kuendesha mauaji ya makundi.

Ripoti ilisikika kutoka kwa maafisa wanaodaiwa kupinga ugaidi, ambao walisema waliwaua washukiwa kwa kufuata maagizo ya serikali.

Serikali ya Kenya ilikataa tuhuma hizo, na kuiita ripoti hiyo “yenye kashfa na isiyo na maadili.”

Makundi ya kutetea haki za binadamu yalishaishtaki Kenya kipindi cha nyuma kwa kufanya mauaji kinyume cha sheria.


Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya imekishtaki kituo cha Al-Jazeera kwa kujaribu “kudhoofisha” jitihada za Wakenya kupambana na wanamgambo.

‘Makala hiyo ilitengenezwa makusudi na kurushwa hewani wakati Kenya ikitafuta msaada wa kuimarisha mapambano yake dhidi ya ugaidi,” wizara ilituma ujumbe wa twitter.

Mauaji ya hali ya juu yaliwalenga Waislamu wenye msimamo mkali, wakiwemo wale wanaohusishwa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab, kwa mujibu wa ripoti.

Pia ripoti hiyo ilituhumu kuwa mashirika ya kijasusi ya kimagharibi yalitoa baadhi ya taarifa zilizohitajika kufanya mauaji hayo.

Chanzo: taarifa.co.tz

No comments:

Post a Comment