Sunday, 7 December 2014
IDRIS ASHINDA BIG BROTHER AFRIKA 2014
Idris Sultan mwenyeji wa Arusha, Tanzania mwenye umri wa miaka 21 anajieleza kama hodari, mcheshi, mchangamfu na mbunifu ameibuka kidedea katika shindano la Big Brother Afrika 2014.
Anapenda miondoko mbalimbali ya muziki, na wasanii wanaomvutia zaidi ni Chris Brown, Michael Jackson, Usher, Ed Sheeran, Sam Smith, Lana Del Ray na Nina Simone.
Idris anasema hana mtu mmoja tu anayemvutia ‘role model’ badala yake huvutiwa na mtu mmoja mmoja kwa kila jambo, huku akiongeza kuwa mama yake amechangia pakubwa katika maisha yake.
Idris anaondoka na kitita cha dola za Kimarekani elfu 300.
Mwaka 2001 Mtanzania mwengine Richard Dyle Bezuidenhout alishinda shindano hilo, hivyo kumfanya Idris kuwa Mtanzania wa pili kunyakua taji hilo tangu mashindano hayo kuanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment