Monday 8 December 2014

RAIS KABILA AUNDA SERIKALI YA UMOJA, DRC


Joseph Kabila at the UN

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, ametangaza kuwa na serikali mpya itakayojumuisha wanachama kadhaa wa upinzani.

Mwanachama mwandamizi wa chama cha upinzani cha Movement for the Liberation of Congo ametajwa kuwa makamu wa waziri mkuu.

Wengine wengi waliokuwa wapinzani nao pia wamepewa nafasi mbalimbali.

Serikali hiyo ya umoja inaundwa huku kukiwa na hisia kuwa Bw Kabila, ambaye yupo madarakani tangu mwaka 2001, anaweza kujaribu kubadili katiba ili agombee kwa muhula wa tatu.

Wachambuzi wamesema kuwaingiza wanachama kutoka upinzani na waliokuwa wapinzani katika uongozi wake wa sasa huenda ikawa jaribio la kuimarisha ufuasi wake na kugawanya tayari upinzani ulio dhaifu.

Wanasema huenda ikawa ni kujiandaa kwa kubadili katiba au kucheleweshwa kwa uchaguzi mwaka 2016.

Evariste Boshab, kiongozi wa chama tawala cha People's Party for Reconstruction and Democracy na wakili anayezungumza kwa ushupavu kuhusu mabadiliko ya kikatiba, ametajwa naye pia kuwa makamu waziri mkuu.
 

No comments:

Post a Comment