Wednesday, 10 December 2014
SERIKALI RUKHSA KUKATA RUFAA KESI YA PISTORIUS
Jaji wa Afrika kusini ametoa uamuzi kuwa waendesha mashtaka wanaweza kukata rufaa dhidi ya kosa la kuua bila kukusudia, "culpable homicide" ya mwanariadha Oscar Pistorius.
Mwanariadha huyo alipata hukumu ya kifungo cha miaka mitano mwezi Oktoba kwa kumpiga risasi na kumwuua mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana.
Jaji Thokozile Masipa alisema waendesha mashtaka hawawezi kuhoji urefu wa hukumu aliopewa Pistorius.
Mawakili wa Pistorius walipinga ombi la kukata rufaa.
Waendesha mashtaka wanataka ashatakiwe kwa kuua na kesi hiyo sasa itafikishwa katika Mahakama kubwa ya rufaa ya Afrika kusini.
Walisema Jaji Thokozile Masipa alitafisiri sheria tofauti alipotoa hukumu kuwa Pistorius hakumwwia Bi Steenkamp kwa kukusudia.
Jaji Masipa alitoa uamuzi huo mjini Pretoria siku ya Jumatano
Akizungumza siku ya Jumanne, mwendesha mashtaka Gerrie Nel alisema hukumu ya jaji “ni yenye kushtua na isiokubalika na haiendani na uhalifu wenyewe na mshtakiwa mwenyewe”
Waandishi wanasema rufaa hiyo inaonekana kufanyika mwakani.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment