Thursday 11 December 2014

CHINA YACHUNGUZA MAHARUSI 'WALIOTOWEKA'


This photo taken on 29 July 2014 shows two Vietnamese brides embracing in a shop in Weijian village, in China's Henan province.

Serikali ya China inachunguza kutoweka kwa zaidi ya wanawake 100 wa Vietnam katika jimbo la Hebei kaskazini mwa nchi hiyo, vyombo vya habari nchini humo vimesema.

Wanawake hao waliozeshwa kupitia mtu anayewaunganisha na wanaume ‘matchmaker’ wanaoishi vijijini karibu na Handan, lakini alitoweka mwezi Novemba, ripoti hiyo ilisema.

Mwuunganishaji huyo, mwanamke wa Vietnam anayeishi China, naye ameingia mitini.

Uwiano wa wanawake na wanaume China mara nyingine husababisha wanaume makapera walio maskini kutafuta maharusi kutoka nchi za kusini mashariki mwa Asia.

Makapera hao kila mmoja amelipa maelfu ya yuan kwa mwuunganishaji huyo wa Vietnam, ambaye anajulikana kwa jina la Wu Meiyu, aliyekuwa akiishi Hebei kwa zaidi ya miaka 20.

Mapema mwaka huu alitembelea vijiji mbalimbali huko Hebei akitafuta wateja, akiwaahidi kuwapa mke kutoka Vietnam kwa malipo ya yuan 115,000 ($18,600; £11,800), ripoti hiyo ilisema.

Novemba 20, wake waliwaambia waume zao kuwa walikuwa wanaenda kula chakula na maharusi wengine wa Vietnam

Ghafla wakawa hawapatikani.

Waume hao walipoenda nyumbani kwa Bi Wu kukabiliana naye, waligundua aliondoka siku chache zilizopita.

No comments:

Post a Comment