Thursday, 11 December 2014

MTOTO WA ZUMA ALAUMIWA KUUA


 South African President Jacob Zuma's son Duduzane Zuma at the Randburg Margistrate Court on 4 November 2014

Maulizo nchini Afrika kusini imegundua mtoto wa kiume wa Jacob Zuma hakuwajibika katika ajali ya gari iliyosababisha kifo cha mwanamke mmoja.

Waendesha mashtaka mwanzo waliamua kutomshtaki, lakini sasa watashinikizwa kufanya hivyo, waandishi walisema.

Gari la Duduzane Zuma aina ya Porsche liligonga gari aina ya minibus kwa nyuma mjini Johannesburg mwezi Februari, na kumwuua mwanamke huyo hapo hapo.

Rais huyo ana watoto 21 na ameoa mara sita.

Bw Duduzane , mwenye umri wa miaka 30, alijieleza kwenye kamati hiyo ya maulizo kuwa aliyumba na gari hilo baada ya kuingia kwenye mtumbwi.

Hatahivyo, hakimu mkazi Lolita Chetty alitoa uamuzi kuwa “hakuonyesha nidhamu  kulingana na hali iliyokuwepo.”

Mwezi Julai, Mamlaka ya Mashtaka ya Taifa (NPA) yalikataa kumfungulia mashtaka mfanyabiashara huyo ya mauaji bila kukusudia, yakisema hamna ushahidi wa kutosha.

Watu wengine watatu walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Chanzo:BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu


No comments:

Post a Comment