Friday, 26 December 2014

MADEREVA WA KIKE SAUDIA WASHTAKIWA 'KIGAIDI'



 Loujain al-Hathloul at wheel of her car

Wanawake wawili kutoka Saudi Arabia waliotiwa kizuizini kwa kukiuka amri ya kupigwa marufuku kwa madereva wanawake, sasa kesi yao itasikilizwa kwenye mahakama ya ugaidi, wanaharakati walisema.

Loujain al-Hathloul, mwenye umri wa miaka 25, na Maysa al-Amoudi, 33, wamekuwa kizuizini kwa takriban mwezi mzima.

Kesi za wanawake hao zinaripotiwa kuhamishwa kutokana na maneno waliyoandika kwenye mitandao ya kijamii – badala ya kuendesha kwao magari, kulingana na wanaharakati.

Saudi Arabia ni nchi pekee duniani kukataza wanawake kuendesha gari duniani.

Wanaume pekee ndio hupewa leseni ya udereva – na wanawake wanaoendesha gari hadharani huwa hatarini kutozwa faini na kukamatwa na polisi.

Wanawake wa Arabuni wamefanya kampeni nyingi – zikiwemo kwenye mitandao ya kijamii – kutaka vizuizi vipunguzwe.

No comments:

Post a Comment