Tuesday, 23 December 2014

MUUZAJI 'KINARA' WA PEMBE ZA NDOVU AKAMATWA TZ



African elephant

Mfanyabiashara wa Kenya anayeshukiwa kuhusika na ujangili wa kimataifa wa pembe za ndovu amekamatwa nchini Tanzania.

Polisi walisema Feisal Mohamed Ali alihusishwa na mauzo ya tani tatu za meno ya tembo mjini Mombasa nchini Kenya.

Bw Ali alijificha kwa miezi kadhaa na alikuwa katika orodha ya Shirika la Polisi la Kimataifa, Interpol la wanaosakwa kwa uuzaji haramu wa pembe za ndovu.

Uwindaji haramu wa tembo umeongezeka barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni, sababu moja ikiwa imechochewa na China kutaka bidhaa hiyo.

Mwezi Juni, polisi wa Kenya walifanya uvamizi na kugundua pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi ya tembo 100 waliouawa.

Tangu wakati huo Ali amekuwa mbioni, kulingana na shirika la habari la AFP, na kuorodheshwa kama “mhalifu wa kimazingira” na Interpol kabla ya kukamatwa.

Shirika la Wanyamapori Kenya limesema wawindaji haramu wameua tembo 142 nchini humo kwa mwaka huu pekee.

Msemaji mmoja alisema idadi hiyo imepungua kutoka 302 mwaka jana, sababu moja ikiwa ni  kutokana na sheria za kupinga uwindaji haramu.

Lakini nchini Tanzania, Bw Ali alipokamatwa, takriban tembo 10,000 waliuawa mwaka jana.

Chanzo: BBC
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu


1 comment: