Thursday, 25 December 2014
OMBAOMBA APIMWA IMANI, KAFAULU?
Mtu mmoja kutoka California aliyedhamiria kuona ombaomba atafanya nini akigaiwa dola 100, alipatwa na mshangao mkubwa baada ya hatua hiyo.
Josh Paler Lin maarufu katika mtandao wa YouTube — ambaye amejulikana zaidi kwa video zake za maskhara –aliweka video hiyo siku ya Jumatatu, inayoanza akimpa ombaomba huyo pesa hizo mjini Los Angeles, halafu wakianza kumfuatilia kisiri mtu huyo huku wakimrekodi.
Ombaomba huyo, anayejulikana tu kwa jina la Thomas alipoingia kwenye duka linalouza pombe, Paler Lin aliamini kashapata jibu alilolitaka.
Hatahivyo, Thomas aliingia humo kununua chakula, halafu kuelekea eneo ambalo ombaomba wengine wengi hukusanyika na kuanza kuwagawia chakula hicho.
'Sikutarajia kurekodi kitu kama hichi... kusema ukweli, nilidhani ingekuwa mwanzo wa kufichua tabia za ombaomba,’ Paler Lin aliandika kwenye ukurasa wake wa YouTube.
'Nina furaha sana nimeweza kushuhudia na kurekodi tukio la kipekee.
'Sijamsaidia tu ombaomba, lakini nimeweza kukutana na binadamu wa aina yake na rafiki.
'Tulikuwa tukimfuatilia kwa takriban saa moja nzima.'
Thomas alimwambia Paler Lin aliacha kazi yake ili kuwatunza wazee wake, lakini baada ya wote wawili kufariki, hakuwa na uwezo wa kulipia nyumba na kujikuta yupo mtaani.
Paler Lin pia ameanzisha ukurasa maalum wa kukusanya fedha kwenye Indiegogo kwa ajili ya Thomas, kwa matumaini ya kupata $10,000 kwa ajili yake.
Ukurasa huo tayari umeshachangisha zaidi ya dola 35,000.
Kutazama video hiyo bonyeza hapa http://dailym.ai/1rk67Qr
Chanzo: dailymail.co.uk
Imetafsiriwa na Mwandishi wetu
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment