Sunday, 28 December 2014
GEORGE WEAH ASHINDA USENETA LIBERIA
Aliyekuwa nyota wa soka George Weah ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa seneta nchini Liberia, kwenye uchaguzi uliovurugwa na mlipuko wa Ebola.
Bw Weah alipata 78% ya kura zote kwa kiti cha kaunti ya Montserrado, ukiwemo mji mkuu Monrovia.
Alimshinda Robert Sirleaf, mtoto wa kiume wa Rais Ellen Johnson Sirleaf, ambaye alipata takriban 11%.
Idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura, ambao mwanzo ulipangwa kufanyika mwezi Oktoba, ulitokana na wasiwasi wa kuenea kwa Ebola.
Udhibiti mkali wa kiafya uliwekwa kuzuia usambazaji wa ugonjwa huo.
Wengine walioshinda katika uchaguzi huo wa seneta ni pamoja na Jewel Howard-Taylor, aliyekuwa mke wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo aliyopo gerezani kwa sasa Charles Taylor, na aliyekuwa kiongozi wa waasi Prince Johnson. Wote wawili wamebaki na nafasi zao.
Bw Weah alishinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2005, na kushindwa duru ya pili ambapo nafasi hiyo alipata Bi Johnson-Sirleaf.
Ni Mwafrika pekee kutajwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa, aliposhinda mwaka 1995.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment