Saturday, 13 December 2014
MUME 'NJE' KISA, MSHAHARA WA MKE HAUTOSHI
Mwanamme mmoja huenda akafukuzwa kutoka Uingereza baada ya jaji mmoja kutoa uamuzi kuwa mshahara wa mke wake aliye Mwingereza hautoshi.
Michael Engel, kutoka Afrika kusini, alisema sheria za mfumo mzima wa uhamiaji “wa ajabu” ulikuwa “ukiwashambulia raia wa Uingereza”.
Bw Engel, mhandisi wa boti mwenye umri wa miaka 31 anayeishi Cornwall, alisema yeye na mkewe Natalie wana mpango wa kurudi Afrika kusini na mtoto wao wa kike aitwaye Nyana mwenye umri wa miezi 18 .
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Uingereza alisema sheria hizo zimeundwa kuzuia wanandoa wa kigeni kutegemea pesa za walipa kodi wa nchi hiyo.
'Nimeshtushwa mno'
Wanandoa hao waliambiwa kuhusu uamuzi huo wa uhamiaji baada ya kukata rufaa kwa misingi ya haki za binadamu kwa nia ya kulinda familia yao.
Lakini kwa sheria zilizoanzishwa mwaka 2012, raia wa Uingereza wanaotaka kuleta mwenza kutoka nchi za kigeni lazima wawe na mshahara wa £18,600 kwa mwaka na nyingine £3,800 – jumla £22,400 – iwapo wenza hao wana mtoto.
Biashara ya uchongaji ya Bi Engel's ilizalisha £19,786 mwaka 2014 ambapo jopo la waamuzi waliamua kuwa kiwango hicho hakitoshi.
Natalie alisema: "Nimeshtushwa mno, nimeishiwa la kusema, nina hasira. Sioni fahari kuwa Mwingereza kwa sasa."
Wenza hao wana siku 14 kukata rufaa kuhusu uamuzi huo.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment