Sunday, 14 December 2014

AFRIKA YANYAKUA 'MISS WORLD 2014'



Rolene Strauss wa Afrika kusini ametwaa taji la Mrembo wa Dunia ‘Miss World 2014’, akimrithi Megan Young wa Ufilipino kwa nafasi hiyo katika shughuli iliyofanyika kituo cha ExCeL Exhibition mjini  London.

Mrembo huyo mwenye umri  wa miaka 22 amekonga nyoyo za wengi kutokana pia na hali ya kuwa mwanafunzi wa udakatari kwenye nchi aliyotoka.

"Afrika Kusini hii ni kwa ajili yenu," Strauss alisema baadae.

Aliongeza pia, "Ni jukumu kubwa."

"Natumai Mrembo wa Afrika Kusini atafurahia taji hilo kwa mwaka mzima kama mie," alisema Young.
Wakati huohuo, Young alikuwa binti wa kwanza kushinda taji hilo la Mrembo wa Dunia kutoka Ufilipino mwaka jana.

Edina Kulcsar wa Hungary amekuwa wa pili, wakati Mmarekani  Elizabeth Safrit amekuwa wa tatu.


“Urembo wenye Malengo”


Kipengele cha mashindano ya Urembo wenye Malengo, “Beauty with a Purpose” ni pale washindani wanapoangaliwa kwa misingi ya mchango wao kwenye jamii.

Kwa mara ya kwanza si mmoja bali watano wametangazwa kushinda katika misingi hiyo.

Washindi hao ni Miss India, Miss Kenya, Miss Brazil, Miss Indonesia na Miss Guyana.

Mrembo wa Dunia kutoka Kenya 2014 Idah Nguma amefanya kazi ya kuwashawishi wazazi wenye watoto wanaosumbuliwa na ‘cleft clip’ kufanyiwa upasuaji.

Tatizo hilo ambalo linawakumba wengi Kenya, huacha mdomo wa juu wa mtoto ukiwa umekatika katikati, na kusababisha mtoto kutoweza kula wala kuongea.

Kulingana na Idah, tatizo hilo huacha watoto wakiwa wametengwa na kunyanyapaliwa na wakati mwengine hata kuuliwa.

Bahati nzuri, tatizo hilo lina tiba na linaweza kurekebishwa kwa kufanyiwa upasuaji mdogo.


No comments:

Post a Comment