Blogger maarufu na mwenye utata wa Kenya amefunguliwa
mashtaka ya kumdhalilisha rais , kufuatia ujumbe wa twitter aliyoweka mapema
wiki hii.
Robert Alai, mkosoaji mkali wa serikali, alimwita Rais Uhuru Kenyatta "adolescent president".
Alikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana kwa dola 2,000 na kuamriwa kutoweka ujumbe unaofanana na huo wakati uchunguzi ukiendelea.
Bw Alai ni miongoni mwa blogger maarufu na wenye ushawishi mkubwa Kenya.
Ana wafuasi 140,000 kwenye ukurasa wake wa twitter.
Siku hiyo aliyomwita rais jina hilo, pia akaweka namba za simu za rais na baadhi ya maafisa waandamizi.
Bw Alai tayari ana wengi wanaomwuunga mkono kwenye mtandao wa kijami wa Twitter kutoka kwa Wakenya wanaoona mashtaka hayo kama mbinu ya serikali ya kuzuia uhuru wa vyombo vya habari.
Alipotolewa tu kwa dhamana, aliandika kwenye twitter kuwa itakuwa ngumu kumnyamazisha.
Miaka miwili ilyopita, alikamatwa na kuhojiwa baada ya kudai kuwa msemaji wa serikali ya wakati huo alikuwa akipanga kumwuua.
No comments:
Post a Comment