Biashara ya
kwanza ya Bima kwa zaidi ya miaka 20 imeanza kwenye mji mkuu Mogadishu nchini Somalia.
Kampuni hiyo (Somali Takaful and Re-Takaful) inayosema inafuata sharia za
Kiislamu itaanza kwa kutoa bima za mota na mizigo ya majini.
Mkurugenzi
wa kampuni hiyo Mohamed Jesow alisema watu wengi Mogadishu hawajui hata bima ni
nini, kwani nchi hiyo imekuwa uwanja wa vita tangu serikali kuu kuporomoka
mwaka 1991.
Alisema
wateja watakaolipwa fidia ni wale ambao mali zao ziliharibiwa kwa bomu na
mashambulio mengine, ilimradi hawakulengwa wao moja kwa moja.
Ulinzi
umeimarika Mogadishu katika miezi ya hivi karibuni, lakini kundi la al-Shabab
na wengine mara nyingi hufanya mashambulio.
No comments:
Post a Comment