Friday 26 December 2014

KESI YA ALIYEKUWA MKE WA RAIS WA I COAST YAANZA



Former Ivory Coast President Laurent Gbagbo and his wife Simone attending a ceremony in Abidjan in 2011
Aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na mkewe walikamatwa mwaka 2001

Kesi ya aliyekuwa mke wa rais wa Ivory Coast, Simone Gbagbo, kwa madai ya kuhusika katika ghasia za baada ya uchaguzi miaka mitano iliyopita imeanza.

Mke wa aliyekuwa Rais Laurent Gbagbo ameshtakiwa pamoja na wafuasi wengine 82 wa mume wake.

Bw Gbagbo anasubiri kesi yake ianze kusikilizwa katika Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC, kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Takriban watu 3,000 walikufa kutokana na ghasia, baada ya aliyekuwa rais kukataa kukubali kushindwa wakati wa marudio ya upigaji kura.

Bi Gbagbo, aliyewekwa kifungo cha nyumbani kwa miaka mitatu, ameshtakiwa kwa “jaribio la kuyumbisha usalama wa taifa”.

Aliyekuwa waziri mkuu Gilbert Ake N'Gbo na mkuu wa chama cha Ivorian Popular Front (FPI) Affi N'Guessan wanashtakiwa pia pamoja na Bi Gbagbo.  

Mume wake, aliyekuwa Rais Laurent Gbagbo, anakabiliwa na mashtaka manne ICC mjini  Hague, ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji na udhalilishaji.

Bw Gbagbo, mwenye umri wa miaka 69, anayesisitiza kuwa hana makosa, ni wa kwanza aliyekuwa rais kufikishwa mahakama ya ICC.


No comments:

Post a Comment