Waliohojiwa Afrika ndio wenye furaha zaidi |
Watu wenye furaha inaongezeka duniani, kulingana na utafiti wa mwisho wa mwaka wa watu 64,000 katika nchi 65.
Shirika lililofanya utafiti huo WIN/Gallup liligundua kuwa 70% ya waliohojiwa wameridhika na maisha yao – idadi iliyoongezeka kwa 10% kutoka mwaka jana.
Fiji ndilo taifa lenye furaha zaidi, huku 93% ya wakazi wakiwa na furaha na kuridhika, na Iraq ikiwa la mwisho lenye furaha kwa 31%.
Utafiti huo umeonyesha kuwa Afrika ni bara lenye furaha zaidi, huku 83% ya watu wakisema wana furaha au furaha sana.
Wakati huohuo, Ulaya ya Magharibi ilionekana eneo lenye watu wengi wasio na furaha, huku 11% wakisema hawana furaha au hawana furaha hata kidogo.
Kwa takwimu za ulimwengu, 53% ya waliohojiwa walihisi mwaka 2015 utakuwa mzuri zaidi kuliko 2014.
Robo tatu ya waliohojiwa Afrika walikuwa na matumaini makubwa ya maisha kuimarika, ikilinganishwa na 26% ya waliopo Ulaya ya Magharibi.
Nigeria ndio nchi yenye hisia chanya kuliko zote, huku Lebanon ikiwa yenye hisia hasi kuliko zote.
No comments:
Post a Comment