Tuesday, 16 December 2014

THIERRY HENRY ASTAAFU SOKA



Henry



Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry ametangaza kujiuzulu soka baada ya kudumu kwenye fani hiyo kwa miaka 20 na kuingia kwenye taaluma ya habari.

Mchezaji aliyekuwa katika timu ya taifa iliyoshinda kombe la Dunia mwaka 1998, mwenye umri wa miaka 37, aliondoka New York Red Bulls mwezi huu huku kukiwa na hisia huenda akaamua kwenda kuchezea timu nyingine.

“Imekuwa safari ya kipekee,” alisema.

Henry anajiunga na Sky Sports baada ya kuwa mchambuzi wakati wa Kombe la Dunia na BBC.

Mchezaji huyo kutoka Ufaransa, ambaye pia aliichezea Juventus, Barcelona na Monaco, alifunga magoli 175 ya Ligi Kuu ya England na yuko nafasi ya nne kwa wafungaji wa magoli mengi.


Thierry Henry
Henry akisherehekea na wenzake wa Barcelona, Sylvinho na Lionel Messi after the 2009 Champions League final


Henry alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya England na matatu ya Kombe la FA akiwa na the Gunners, ambapo alicheza kati ya mwaka 1999 na 2007.

Aliongeza tuzo ya Ligi ya Ulaya akiwa na Barcelona mwaka 2009 na kurejea Arsenal kwa ajili ya mechi nne kwa mkopo kutoka Red Bulls mwaka 2012.


                                                                

No comments:

Post a Comment