Sunday, 14 December 2014
BOLIVIA YAPAMBANA NA 'MAAFISA WANENE'
Majeshi ya usalama ya Bolivia yameanza kusajili wenye uzito mkubwa baada ya Rais Evo Morales kulalamika kuwa wengi wao hawana mwonekano mzuri.
Maafisa wa usalama wamesema wataanza kupima uzito kwanza kabla ya kufanyiwa mitihani ya kitaaluma, ili kuimarisha afya na namna ya kupandisha vyeo.
Waziri wa Ulinzi Ruben Saavedra alisema wanajeshi "lazima wajiandae kwa viwango vyote viwili afya na taaluma".
Polisi imewakataza wanachama wenye uzito mkubwa kuvaa sare za jeshi mpaka wapungue.
Hatua hiyo tayari huenda imeonekana kuzaa matunda.
Mjini Oruro kusini mwa La Paz, polisi waliokuwa wakipiga doria na nguo za nyumbani walifanikiwa kukamata wezi kwenye soko moja, infahamika ni kwasababu hawajavaa sare zao.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment