Friday 19 December 2014

UCHUNGUZI MPYA WAONYESHA EBOSSE ALIPIGWA



 Albert Ebosse ceremony

Uchunguzi mpya wa mwili wa mcheza soka wa Cameroon Albert Ebosse unaonyesha kuwa kifo chake ni matokeo ya kupigwa badala ya taarifa ya awali kuwa alitupiwa kitu, ‘projectile’.

Mfungaji huyo wa JS Kabylie alikufa mwezi Agosti baada ya timu yake kushindwa.

Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Algeria zilisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliuawa na kitu chenye ncha kali kilichorushwa na mashabiki.

Lakini mchunguzi wa seli Andre Moune ameiambia BBC World TV: "Ukiona majeraha kwenye mabega yake, namna pekee ya kuelezea ni kuwa alishambuliwa.”

Cameroon imefanya uchunguzi huo baada ya kuombwa na familia ya Ebosse.

Aliripoti kuwa mwanasoka huyo “alipata pigo kubwa kichwani” iliyosababisha fuvu kubonyea” na kuathiri ubongo na pia alikuwa na majeraha sehemu ya juu ya mwili inayoashiria “ishara za kupambana”.

Matokeo ya uchunguzi wake yamepelekwa kwenye mamlaka za Algeria na Cameroon kwa hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment