Viongozi wa NATASA. Kutoka kushoto katibu mkuu Halima Guga, Mwenyekiti Given Massawe, Mratibu wa Elimu Abdulkarim Baksh
Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang nchini
China wameanzisha umoja wao na jana Jumamosi wameuzindua rasmi umoja huo
wenye lengo la kuwasaidia kwa mambo mbalimbali wakiwa kwenye nchi ya
kigeni.
Jumla ya wanafunzi 54 wa Kitanzania wapo kwenye mjii huo
wakiwa wanasoma kwenye vyuo mbalimbali na walikuwa hawana kitu
chochote kinachowaweka karibu kama Watanzania na ndio maana wakaanzisha
umoja huo.
Umoja huo unaojulikana kwa jina la Nanchang, Tanzanian
Students Association (NATASA) ulizinduliwa ramsi na mwenyekiti wake
Given Massawe ambae alisema kuanzishwa kwa umoja huo lilikuwa ni wazo la
muda mrefu na hatimae hivi sasa ndoto imetimia.
Massawe
alifafanua kuwa kwenye mijii mbalimbali mingine ya nchini China ambako
kuna wanafunzi wa Kitanzania nao wanajumuia zao ambazo zinawasaidia
hivyo kwa wanafunzi wa Nanchang kuwa na umoja huo ni sehemu ya kufungua
milango kwao.
Mwenyekiti huyo amesema hivi sasa wapo kwenye
harakati ya kutengeneza katiba yao ambayo ndio itakuwa dira ya uongozi
wao na pia kuzinduliwa kwa chama hicho ni msaada tosha kwa wanafunzi hao
wa Kitanzania kuanzia kwenye masomo hadi maisha ya kila siku.
Uzinduzi
wa umoja huo ulienda sambamba za sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa
Tanzania bara na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa
Nanchang kusherekea siku yao ya Uhuru wakiwa pamoja.
Taarifa kutoka Mo van der Mhando Nanchang, China.
Kwa picha zaidi bonyeza hapo
| | | | | | |
No comments:
Post a Comment