Sunday 7 December 2014

RAIS MUGABE NA MKEWE WOTE WATAMBA, ZIMBABWE



 

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amechaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama hicho, wakati mke wake Grace amepewa nafasi ya juu katika chama hicho.

Kupandishwa cheo kwa Grace Mugabe kuongoza jumuiya ya wanawake wa chama cha Zanu-PF inamweka katika nafasi nzuri ya kumrithi mumewe siku za usoni, wachambuzi wanasema.

Mke huyo wa Mugabe amewakosoa wapinzani wa kisiasa, akiwemo makamu wa Rais Joyce Mujuru, katika miezi ya hivi karibuni.

Bw Mugabe, mwenye umri wa miaka 90, anatarajiwa kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi tena mwaka 2018.

Akizungumza katika mkutano wa Zanu-PF, Bw Mugabe aliwashukuru maelfu ya wafuasi wake kwa kumchagua kuwa kiongozi wa chama hicho.

"Najua nilipotoka... mimi sipo juu ya watu walionizaa,” Bw Mugabe aliyeiongoza Zimbabwe tangu mwaka 1980, alisema.

Rais wa Zimbabwe amezungumzia hasira zake juu ya naibu wake walio kwenye mzozo Joyce Mujuru kwa madai ya kula njama ya kumwuua kiongozi huyo na kumtuhumu kuwa mwizi.

Akizungumza katika mkutano wa chama tawala cha Zanu-PF, Robert Mugabe alisema atawashughulikia maafisa wote mafisadi.

Kutokuwepo Bi Mujuru kwenye mkutano huo kunaashiria kuwa “anaogopa” alisema Bw Mugabe.

Siku za hivi karibuni mwanachama wa Zanu-PF aliyefurumushwa Rugare Gumbo aliiambia  BBC kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 90 amebadilisha “kabisa” chama hicho kuwa “mali yake binafsi”.

Bw Mugabe alimlenga Bi Mujuru ili ‘kumpembejea’ mke wake Grace, aliyekuwa msemaji wa Zanu-PF aliongeza.

Bi Mujuru, ambaye hivi karibuni alikana madai hayo, alikuwa ana nafasi kubwa ya kumrithi Bw Mugabe, ambaye alikuwa naye sambamba wakati wa kupigania uhuru wa Zimbabwe kutoka kwa wazungu walio wachache.

Hatahivyo, ndoto zake zilianza kuyumba baada ya Bi Mugabe kuingia kwenye siasa mwaka huu, na kumshutumu kwa kupanga jaribio la kumwuua mumewe.

No comments:

Post a Comment