Kenya imeimarisha usalama kufuatia mashambulio na wanamgambo |
Kenya imewafutia usajili mashirika yasiyo ya kiserikali
510 (NGOs), wakiwemo watuhumiwa watano wanaohusishwa na ugaidi, afisa mmoja
alisema.
Serikali pia imepiga tanji akaunti zao za benki na kufuta
vibali vya kazi vya wafanyakazi wa kigeni.
Hatua hiyo inafuatia mjadala mzito nchini Kenya juu ya
mswada mpya tata wa usalama wenye lengo la kupambana na wapiganaji.
Kundi la al-Shabab linalohusishwa na al-Qaeda limezidi
kufanya mashambulio Kenya.
Mashirika hayo yalifutiwa usajili wao kutokana na
kushindwa kuwasilisha rekodi zao za fedha, alisema Henry Ochido, naibu mkuu wa
bodi ya NGOs iliyoteuliwa na serikali, inayosimamia shughuli zao.
Bw Ochido aliiambia BBC, 15 wanatuhumiwa kwa magendo na
kufadhili “ugaidi”.
Baadhi walihusishwa na mashambulio mawili ya mabomu ya mwaka 1998 ya balozi za Marekani nchini Kenya na nchi jirani ya Tanzania, alisema.
Bw Ochido alikataa kutaja majina ya mashirika hayo, akisema uchunguzi bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment