Tuesday 2 December 2014

AL-SHABAB YAUA TENA KENYA


Protests in Nairobi, 25 November 2014
Maandamano makubwa yalifanyika wiki iliyopita kufuatia shambulio katika basi karibu na eneo hilo hilo

Wapiganaji wa Al-Shabab wamewaua watu 36 wengi wakiwa Wakristo wanaofanya kazi kwenye machimbo karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa nchi ya Kenya.

Washambuliaji hao wenye makao makuu yao Somalia waliwatenganisha Waislamu na wasio waislamu na kuwapiga risasi za kichwa Wakristo, kulingana na wakazi wa eneo hilo.

Awali, mtu mmoja aliuawa katika baa maarufu kwa wasio Waislamu kwenye wilaya jirani.

Al-Shabab iliwaua watu 28 katika shambulio la basi lililowalenga wasio waislamu katika eneo hilo hilo wiki iliyopita.

Shambulio kwa wachimbaji hao lilifanyika siku ya Jumanne.

Walioshuhudia walisema watu hao walikamatwa saa sita za usiku, wakiwa wamelala kwenye maturubali katika machimbo hayo.

Shambulio hilo lilifanyika ormey, kilomita 15 kutoka mji wa Mandera.

Mtu mmoja aliyetembelea eneo hilo aliiambia BBC baadhi ya waliouawa inaonyesha kama walilazwa chini, na kupigwa risasi kichwani.

Wengine wanahisi maturubali ya wafanyakazi hao yalimiminiwa risasi.

Al-shabab imesema imehusika na mauaji hayo.

                                                                                                   

No comments:

Post a Comment