Saturday, 13 December 2014
YAYA WA UGANDA AKUTWA NA HATIA
Mfanyakazi wa ndani nchini Uganda ambaye alirekodiwa kwa siri hivi karibuni akimpiga mtoto mdogo wa kike amekutwa na hatia ya kumnyanyasa binti huyo.
Jolly Tumuhirwe, mwenye umri wa miaka 22, ameiambia mahakama kuwa kilichomchochea kumpiga mtoto huyo wa miezi 18 ni kufuatia mama wa mtoto huyo kumpiga- jambo ambalo mama wa mtoto huyo amelikataa.
Video ya unyanyasaji huo ulisababisha hasira kali miongoni mwa wengi ilipowekwa kwenye mitandao ya kijamii.
Awali mashtaka ya utesaji yalifutwa baada ya waendesha mashtaka kusema si rahisi kuthibitisha hilo.
Tumuhirwe sasa anakabiliwa na mpaka kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kumnyanyasa mtoto huyo na kumsababishia maumivu mwilini.
Hukumu yake inatarajiwa kutolewa siku ya Jumatatu.
Labels:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment