Tuesday, 9 December 2014

VIFO KUTOKANA NA MALARIA VYAPUNGUA KWA NUSU



Mosquito

Jitihada za dunia zimepunguza nusu ya watu wanaokufa na malaria – ambapo ni mafanikio makubwa, kulingana na Shirika la Afya Duniani WHO.

Linasema kati ya mwaka 2001 na 2003, vifo milioni 4.3 vimezuiwa, ambapo milioni 3.9 miongoni mwao ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano eneo la kusini mwa jangwa la Sahara.

Kila mwaka, watu wengi zaidi wanapata dawa za kuwakinga na malaria, WHO limesema.

Mwaka 2004, 3% walio hatarini kupata ugonjwa huo walikuwa na uwezekano wa kupata chandarua, lakini sasa ni 50%.

Kushinda mapambano

Idadi ya watu wanaopima imeongezeka, na watu wengi zaidi wana uwezo wa kupata dawa kutibu vijidudu vya malaria, inayosambazwa na kung’atwa na mbu mwenye vidudu hivyo.

Nchi nyingi sasa zinaelekea kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.


child sleeping under a bed net

Mwaka 2013, nchi mbili - Azerbaijan na Sri Lanka – waliripoti kutokuwepo na mgonjwa hata mmoja wa maradhi hayo kwa mara ya kwanza, na nyingine 11 (Argentina, Armenia, Misri, Georgia, Iraq, Kyrgyzstan, Morocco, Oman, Paraguay, Turkmenistan na Uzbekistan) nao wamefanikiwa kutokuwa na kesi mpya.  

Barani Afrika, ambapo 90% ya vifo vyote vya malaria hutokea hapo, imepungua kwa kiwango kikubwa.

Idadi ya watu waliopata maradhi hayo barani humo imepungua kwa robo – kutoka watu milioni 173 mwaka 2000 hadi milioni 128 mwaka 2013.

Hii ni licha ya ongezeko la 43% ya idadi ya watu barani Afrika wanaoishi maeneo yaliyo rahisi kupata maradhi hayo.

No comments:

Post a Comment