Monday, 1 December 2014

MUHAMMAD: MAARUFU KWA WATOTO WA KIUME, UK



Muhammad limekuwa jina maarufu kwa watoto wa kiume nchini Uingereza, mtandao wa BabyCentre umedai.

Wakati huohuo majina ya kiarabu yamezidi kutumika zaidi.

Vipindi vya televisheni kama vile Game of Thrones pia vimechangia sana kutoa majina ya kizazi kijacho.

Orodha ya majina 100 bora ya watoto kwa mwaka 2014 imeonyesha Muhammad imepanda nafasi zaidi ya 27 kutoka mwaka jana hadi kufika namba moja.

Jina hilo limepata nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na watu 56,157 wa wanachama wa mtandao wa BabyCentre.co.uk waliojifungua mwaka 2014.

Kwa ujumla kumekuwa na ongezeko kubwa la majina ya kiarabu, huku Nur likiwa jipya kuingia katika orodha hiyo katika majina 100 bora ya kike, likiruka hadi nafasi ya 29, na Maryam likipanda mara 59 na kuchukua nafasi ya 35.

Omar, Ali na Ibrahim ni majina mapya kuingia katika 100 bora za kiume.

Sophia ndio namba moja katika majina ya watoto wa kike, na kupata umaarufu tena katika orodha ya mtandao wa BabyCentre nchini Marekani, Brazil, Hispania na Urusi mwaka jana.

Lakini jina linalotamba zaidi upande wa watoto wa kike ni Maryam, huku majina mapya zaidi ni Nur, Emilia na Gracie.

Chanzo: www.theguardian.com

HOTELI CHINI YA BAHARI KISIWANI PEMBA, TANZANIA

   
Ushawahi kufikiria kulala na samaki? Au kuzungukwa na samaki. Hoteli ya kwanza chini ya maji barani Afrika imefunguliwa kisiwani Pemba nchini Tanzania. Hoteli hiyo ina umbali wa mita 250 kutoka baharini. Salim Kikeke katika matangazo ya BBC Dira ya Dunia anasimulia akiwa kisiwani humo.

NDOA YA WATU WENGI KWA MPIGO YAFUNGWA BRAZIL



Mass wedding in Rio de Janeiro

Takriban wapendanao 2,000 nchini Brazil wameoana katika eneo moja mjini Rio de Janeiro, kwenye harusi kubwa ya watu wengi kwa pamoja iliyoweka historia mjini humo.

Tukio hilo la kila mwaka, linalopigiwa chapuo na mamlaka za eneo hilo, lina nia ya kusaidia wapendanao wenye kipato kidogo wasio na uwezo wa kulipia gharama za harusi.


Mamlaka za Rio zilikodisha treni maalum kwa ajili ya wapendanao hao na wageni wao waalikwa.

Takriban watu 12,000 walihudhuria shughuli hiyo katika uwanja wa Maracanazinho.

Majaji walijitolea kuidhinisha shughuli hiyo.



Mass wedding in Rio de Janeiro
Watarajiwa wenye kipato cha dola 640 kwa mwezi waliruhusiwa kufungishwa ndoa kwenye shughuli hiyo 

Wapendanao hao pia walifungishwa ndoa iliyobarikiwa na askofu wa Kikatoliki na padri pia.

Tukio hilo limepewa jina la Dia do Sim", au "Siku ya Nakubali” yaani “I Do Day".

Wengi walioozeshwa walikuwa wakikaa pamoja kwa muda mrefu.

Bw Moraes amekuwa na Ana Rosangela Azevedo,mwenye umri wa miaka 31, tangu mwaka  2010 na mapema mwaka huu waliamua kuhalalisha mahusiano yao.

Sunday, 30 November 2014

MAVAZI YA MABINTI WA OBAMA YALETA KIZAAZAA



 US President Barack Obama smiles at his daughters Sasha and Malia after he pardoned a turkey during a ceremony at the White House on 26 November 2014 in Washington



Mabinti wa Rais Barack Obama Sasha na Malia wameelezewa na afisa mmoja wa chama cha Republican kukosa heshima na hadhi kutokana na mavazi yao siku ya sherehe za Thanksgiving.

Elizabeth Lauten, mkurugenzi wa mawasiliano wa mbunge wa Republican Stephen Fincher, aliandika kauli hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kauli yake hiyo ilikoselewa na wengi na hatimaye kufutwa.

Bi Lauten ameomba radhi kwa “maneno yake yaliokera.”

Aliwashambulia mabinti hao kutokana na mavazi waliovaa katika shughuli ya kila mwaka iliyofanyika Ikulu ya White House.

Malia, mwenye umri wa miaka 16, na Sasha, 13, walisimama karibu na baba yao siku ya shughuli hiyo.

Bi Lauten alisema mabinti hao wangejitahidi "kuonyesha hadhi kidogo".

"Vaa kama unastahili heshima, sio kama uko baa," aliongeza.

Kauli zake hizo zilisababisha hamaki kwenye mitandao ya kijamii, huku kukiwa na madai kuwa alikuwa “akiwadhalilisha” mabinti hao vijana.

Chanzo: washingtontimes.com

AJERUHIWA KWA CHOO CHA KUIBUKA ARDHINI



A scooter lies in pieces after a public toilet suddenly emerged from the ground

Mtu mmoja katika mji wa Amsterdam amejeruhiwa baada ya choo cha umma kinachomazishwa ardhini kuibuka ghafla  bila kutarajia.

Mtu huyo alijeruhiwa na mfano wa motokari iliyoruka angani kwa inayoitwa choo cha Urilift kilichoibuka ghafla.

Kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini kwa majeraha madogo.

Vyoo hivyo vimezagaa maeneo mengi katikati ya Amsterdam, na huibuka kutoka ardhini usiku kuzuia watu kukojoa mitaani.

Walioshuhudia waliripoti kusikia mlio mkubwa sana wakati wa ajali hiyo.

Mtu mmoja aliweka picha baada ya tukio hilo katika mtandao wa kijamii wa twitter na kuandika : “Nimepita pembezoni mwa mlipuko kama dakika mbili zilizopita. Nahisi nina bahati.”

Haiko wazi nini kilisababisha tukio hilo.

Matokeo ya uchunguzi huo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa juma.


Vyoo vya Urilift hupatikana Amsterdam na katika nchi mbalimbali barani Ulaya.


Chanzo: Independent.co.uk

Saturday, 29 November 2014

MICHEPUKO HII ITAADHIRI WENGI



 Vimbwanga vya WhatsApp

Na habari nyingine:

MALAWI NA TANZANIA BADO ZAZOZANIA ZIWA NYASA