Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

Friday 19 December 2014

UCHUNGUZI MPYA WAONYESHA EBOSSE ALIPIGWA



 Albert Ebosse ceremony

Uchunguzi mpya wa mwili wa mcheza soka wa Cameroon Albert Ebosse unaonyesha kuwa kifo chake ni matokeo ya kupigwa badala ya taarifa ya awali kuwa alitupiwa kitu, ‘projectile’.

Mfungaji huyo wa JS Kabylie alikufa mwezi Agosti baada ya timu yake kushindwa.

Uchunguzi uliofanywa na serikali ya Algeria zilisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliuawa na kitu chenye ncha kali kilichorushwa na mashabiki.

Lakini mchunguzi wa seli Andre Moune ameiambia BBC World TV: "Ukiona majeraha kwenye mabega yake, namna pekee ya kuelezea ni kuwa alishambuliwa.”

Cameroon imefanya uchunguzi huo baada ya kuombwa na familia ya Ebosse.

Aliripoti kuwa mwanasoka huyo “alipata pigo kubwa kichwani” iliyosababisha fuvu kubonyea” na kuathiri ubongo na pia alikuwa na majeraha sehemu ya juu ya mwili inayoashiria “ishara za kupambana”.

Matokeo ya uchunguzi wake yamepelekwa kwenye mamlaka za Algeria na Cameroon kwa hatua zaidi.

Tuesday 16 December 2014

THIERRY HENRY ASTAAFU SOKA



Henry



Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry ametangaza kujiuzulu soka baada ya kudumu kwenye fani hiyo kwa miaka 20 na kuingia kwenye taaluma ya habari.

Mchezaji aliyekuwa katika timu ya taifa iliyoshinda kombe la Dunia mwaka 1998, mwenye umri wa miaka 37, aliondoka New York Red Bulls mwezi huu huku kukiwa na hisia huenda akaamua kwenda kuchezea timu nyingine.

“Imekuwa safari ya kipekee,” alisema.

Henry anajiunga na Sky Sports baada ya kuwa mchambuzi wakati wa Kombe la Dunia na BBC.

Mchezaji huyo kutoka Ufaransa, ambaye pia aliichezea Juventus, Barcelona na Monaco, alifunga magoli 175 ya Ligi Kuu ya England na yuko nafasi ya nne kwa wafungaji wa magoli mengi.


Thierry Henry
Henry akisherehekea na wenzake wa Barcelona, Sylvinho na Lionel Messi after the 2009 Champions League final


Henry alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya England na matatu ya Kombe la FA akiwa na the Gunners, ambapo alicheza kati ya mwaka 1999 na 2007.

Aliongeza tuzo ya Ligi ya Ulaya akiwa na Barcelona mwaka 2009 na kurejea Arsenal kwa ajili ya mechi nne kwa mkopo kutoka Red Bulls mwaka 2012.


                                                                

Thursday 27 November 2014

PELE ALAZWA BRAZIL



 

Nyota wa soka wa Brazil Pele amehamishiwa katika idara maalum kufuatia kupata maambukizi kwenye njia ya haja ndogo.

Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo imesema nyota huyo mwenye umri wa miaka 74 aliyeshinda mara tatu kwenye kombe la Dunia amehamishwa baada ya “kuumwa mara kwa mara”.

Ripoti zilisema Pele, aliyelazwa siku ya Jumatatu, alikuwa katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi.

Pele, mshindi katika Kombe la Dunia mwaka 1958, 1962 na 1970, awali alitolewa hospitalini Novemba 13 baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa mawe kwenye figo.

Inaeleweka kwamba wakati huduma maalum ni zaidi ya huduma ya kawaida, lakini si hatari sana kama ilivyo kwenye chumba maalum cha wagonjwa mahututi, na Mbrazil huyo ambaye bado anaheshimika kama mchezaji wa kipekee kuwepo duniani – bado anaweza kutembelewa na wageni.


Monday 27 October 2014

MLINDA MLANGO WA AFRIKA KUSINI AUAWA






Msako mkali unafanyika kutafua wauaji wa  Kapteni wa soka wa Afrika kusini Senzo Meyiwa, polisi wamesema.

Wametangaza kutoa zawadi ya rand 250,000  (£14,100; $22,800) kwa taarifa zozote zitakazosaidia kukamatwa kwa wanaoshutumiwa kuwa wezi waliompiga risasi na kumwuua.

Imeripotiwa alishambuliwa baada ya wanaume wawili kuingia kwenye nyumba ya mpenzi wake huko Vosloorus, kusini mwa Johannesburg.

Watu hao waliingia na kutaka watoe simu zao za mkononi na mali nyingine. Mwanamme mwengine wa tatu alibaki nje.

Mmoja miongoni mwa wawili hao ameelezewa na polisi kuwa mrefu, mweusi, mwembamba na mwenye rasta, na mwengine ni mfupi, mweusi na mkuza.

Rais Jacob Zuma alitoa salaam za rambirambi kwa mlinda mlango huyo, akisema, “hakuna maneno yanayoweza kuelezea mshtuko taifa limepata kutokana na kifo hicho”.

Wakala wake amemwelezea kuwa mtu asiyekuwa na makuu, aliyetoka katika maisha magumu na kufanikiwa kuwa “shujaa katika jicho la kila mmoja”.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa mlinda mlango wa Orlando Pirates na aliichezea Afrika kusini katika mashindano manne ya mwisho ya mechi za kufuzu kombe la Mataifa Afrika.

Siku ya Jumamosi, alikuwa na klabu yake, walipovuka nusu fainali ya kombe la Ligi la Afrika kusini, baada ya kuinyuka Ajax Cape mabao 4 -1.