Friday, 7 November 2014

EBOLA YAPUNGUA LIBERIA



 A Liberian woman prays for the end of Ebola in Monrovia, Liberia - 31 October 2014

Liberia imeshuhudia punguzo kubwa la idadi ya wagonjwa wapya walioambukizwa Ebola, shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka Medecins Sans Frontieres (MSF) limethibitisha.

Limesema moja ya vituo vyake vinavyotoa matibabu Liberia haina wagonjwa wowote kwa sasa – lakini likaonya bado maambukizi ya Ebola yanaongezeka Guinea na Sierra Leone.

MSF, linaloajiri maelfu ya wafanyakazi Afrika magharibi, linaonekana kuwa shirika bora lenye taarifa sahihi za Ebola.

 Takriban wagonjwa 5,000 kati ya 14,000 wamekufa kutokana na virusi vya ugonjwa huo.

Chris Stokes, Mkuu wa MSF wa masuala ya Ebola, ameiambia BBC kwamba kupungua kwa idadi ya watu walioathirika na virusi vya ugonjwa huo kumetoa fursa kwa wafanyakazi wa afya kuongeza jitihada.

Lakini alisema ugonjwa huo unaweza “kuibuka” tena, akisema Guinea imeanza kuwa na ongezeko la wagonjwa hao tena licha ya maambukizi kutangazwa kudhibitiwa mara mbili.

Ili kudhibiti ugonjwa huo, Bw Stokes aliongeza, inatakiwa idhibitiwe Liberia, Guinea na Sierra Leone kwa mara moja.

UBISHANI: NANI HASA ALIYEMWUUA BIN LADEN?



Retired US Navy Seal Robert O'Neill (file image)
Robert O'Neil anasema yeye ndiye aliyempiga risasiOsama bin Laden  kichwani

Mabishano ya umma yameibuka ya komandoo yupi wa Marekani aliyefyatua risasi iliyomwuua Osama bin Laden, zaidi ya miaka mitatu baada ya kifo cha kiongozi huyo wa al-Qaeda.

Aliyekuwa mwanajeshi wa nchi hiyo Seal Robert O'Neill, mwenye umri wa miaka 38, ameliambia gazeti la the Washington Post katika mahojiano kuwa yeye ndiye aliyefyatua risasi hiyo.

Kauli yake inapingana na ya Matt Bissonnette, mwanajeshi mwengine aliyehusika katika uvamizi, kwenye kitabu chake alichochapisha mwaka 2012.

Kiongozi huyo wa al-Qaeda aliuawa kwenye uvamizi uliofanywa na wanajeshi wa Marekani katika eneo alilokuwa akiishi huko Abbottabad, Pakistan.

Osama bin-Laden addresses a news conference in Afghanistan in this May 26, 1998 file photo.
Osama bin Laden
Aghlabu wanajeshi hao (Navy Seals) hutii sheria ya ukimya linalowakataza kupata sifa yoyote kutoka kwa umma kutokana na hatua walizochukua.

Bw O'Neill, aliyestaafu mwaka 2012, awali alielezea habari yake bila kuonekana sura kwenye jarida la Esquire.

Ilitakiwa ajitambulishe hadharani kwenye mahojiano ya televisheni baadae mwezi huu, lakini taarifa za mahojiano hayo yaliwakasirisha waliokuwa wanajeshi wakati huo.

Bw O'Neill alisema yeye na mwenzake mwengine – ambaye utambulisho wake unabaki kuwa siri – walipanda ngazi mpaka ghorofa ya tatu ya makazi yake Abbottabad, Pakistan, na kumwona Bin Laden akichungulia nje ya mlango mojawapo ya vyumba vya nyumba hiyo.

Thursday, 6 November 2014

KIFO KWA KUJIUA KILA SEKUNDE 40, WHO YASEMA



Man alone

Mtu hufa kwa kujiua kila sekunde 40, kulingana na ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imesema kujiua ni “tatizo kubwa la afya kwa umma” ambao kwa muda mrefu umekuwa jambo lisilozungumzika.

WHO limetaka kupunguza idadi ya watu wanaojiua kwa 10% ifikapo mwaka 2020, lakini limeonya kwamba nchi 28 tu ndio zenye mkakati wa taifa wa kuzuia kujiua.

Wanaharakati wamesema kunatakiwa kutolewe elimu zaidi mashuleni.

WHO limekuwa likifanya tathmini kwa miaka 10 juu ya watu kujiua duniani kote.

Limeainisha kuwa:

  • Takriban watu 800,000 hujiua kila mwaka
  • Ni ya pili kwa sababu za vifo vya vijana wa umri wa miaka 15 hadi 29
  • Walio na umri zaidi ya miaka 70 walikuwa na uwezekano mkubwa wa kujiua  
  • Robo tatu ya vifo hivyo ni katika nchi zenye uchumi wa chini na wa kati
  • Katika nchi tajiri, wanaume mara tatu zaidi ya wanawake hujiua  

Ripoti hiyo imesema kupungua kwa uwezekano wa kupata silaha na kemikali zenye sumu zimeonyesha kupunguza idadi ya wanaojiua.

Na pia kuanzisha mkakati wa kitaifa wa kupunguza watu wanaojiua ulikuwa unafanya kazi vizuri, lakini umeundwa katika nchi chache.

Mwiko

Dr Margaret Chan, mkurugenzi wa WHO, alisema: “Ripoti hii ni wito wa hatua kuchukuliwa kuelezea tatizo kubwa la kiafya kwa umma, ambao umekuwa mwiko kwa muda mrefu.”

Unyanyapaa wa jamii dhidi ya magonjwa ya akili unaonekana kuzuia watu kutafuta msaada ambapo humsababishia mtu kujiua.

Jonny Benjamin, mwanaharakati wa kuelimisha masuala ya kujiua Uingereza, ameiambia BBC: “Nadhani kunatakiwa kuwa na elimu zaidi kuhusu kujiua na namna ya kuwasaidia watu wenye mawazo ya kufanya hivyo, watu wachache sana wanajua la kufanya wakimwona mtu ambaye yuko hatarini kujiua au mwenye mawazo na hisia hizo.

BURKINA FASO WAKUBALIANA SERIKALI YA MPITO



 Interim leader Lt Col Isaac Zida. Photo: 5 November 2014

Vyama vya kisiasa vya Burkina Faso vimekubali kuwa hatua ya mpito ya kisiasa nchini humo idumu kwa mwaka mmoja, ikifuatiwa na uchaguzi Novemba 2015.

Lakini mazungumzo kwenye mji mkuu Ouagadougou yalimalizika bila kuwa na makubaliano ya nani atakuwa kiongozi wa serikali ya mpito.

Jeshi limekuwa likishika hatamu tangu Rais Blaise Compaore alipolazimishwa kuachia madaraka wiki iliyopita baada ya maandamano mazito.

Umoja wa Afrika (AU) siku ya Jumatatu umeipa jeshi wiki mbili kukabidhi uongozi kwa raia au wkabiliane na vikwazo.

Lt Col Isaac Zida – kiongozi wa mpito anayeungwa mkono na jeshi baadae alikubali kufuata makataa (deadline) hayo.

Alikuwa wa pili katika makamanda waliokuwa wakimlinda rais.


Wednesday, 5 November 2014

Tuesday, 4 November 2014

VIFIJO NA VIGELEGELE : NYANI WAOANA INDIA



Monkey wedding in Bihar

Zaidi wa wanakijiji 200 kaskazini mwa India wamehudhuria sherehe ya harusi ya nyani wawili.

Harusi hiyo iliandaliwa na mmiliki wa nyani hao, ambaye alisema nyani wa kiume alikuwa “kama mtoto wake wa kuasili”.

Sherehe hiyo ilifanyika siku ya Jumatatu katika wilaya ya Bettiah kwenye jimbo la Bihar, huku “biharusi” akiwa amevaa gauni la rangi ya machungwa na “bwana harusi” kavaa fulana ya njano.

Nyani huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 13 aitwaye Ramu, na bi harusi wake, nyani wa kike akiitwa Ramdulari, walipandishwa juu ya SUV lililojazwa maua huku pakiwepo mziki.

Mamia ya wanakijiji walisema mtaani kuwashuhudia “wanandoa” hao.

Udesh Mahto, mfanyakazi wa kawaida aliye na watoto wa kiume watatu, alisema Ramu alikuwa “kama mtoto wake mkubwa”.

"Nilitaka kumwozesha yeye mwanzo,"alisema.

Bw Mahto alimleta Ramu kutoka Nepal kama miaka saba iliyopita, na baadae kumnunua Ramdulari kutoka kijiji kengine.

"Mwanzoni walikuwa hawapatani. Lakini baadae wakaanza kupendana, kwahiyo nikaamua kuwaozesha, “ alisema.