TWAWEZA ni shirika lenye nia ya kufanya mabadiliko Afrika Mashariki.
Matokeo haya ni muhtasari uliotokana na Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu ya mkononi maeneo yote Tanzania Bara (Zanzibar haimo kwenye matokeo haya).
Matokeo muhimu yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,445 mwezi Septemba 2014.
Matokeo ya utafiti kwa kifupi ni kama ifuatavyo
Mwananchi mmoja kati ya watatu
(33%) Tanzania Bara hajui ni nani atayekuwa chaguo lake la Rais kwenye uchaguzi
mkuu ujao. Hakuna mgombea hata mmoja anayependwa na wapiga kura kwa zaidi ya
15%. Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Twaweza mwezi Septemba 2014,
anayeongoza ni Edward Lowassa (13%) akifuatiwa na Mizengo Pinda (12%) wote wa
CCM, na watatu ni Dkt. Wilbrod Slaa wa Chadema (11%). Wafuasi wa CCM
walipohojiwa, robo yao (24%) walisema watampigia kura yeyote atakayeteuliwa na
chama.
Ukilinganisha kukubalika kwa vyama, nusu ya Watanzania (51%) wanasema wataipigia kura CCM kwenye uchaguzi wa Rais, na robo moja ya Watanzania (23%) wataipigia kura Chadema. Walipoulizwa watafanya nini kama vyama vya upinzani vitaungana na kusimika mgombea mmoja tu, kama UKAWA ilivyoahidi kufanya, CCM bado inaongoza lakini idadi ya watakaoichagua CCM inapungua hadi chini ya nusu (47%) ya wananchi wote. Wakati huohuo, karibu wananchi watatu kati ya kumi (28%) wamesema wangempigia kura mgombea wa upinzani. Idadi kubwa ya wananchi, mmoja kati ya watano (19%) amesema hatapigia kura chama bali mgombea. Ikitokea kundi hili likaamua kumpigia kura mgombea wa upinzani, ushindani utakuwa mkali mwaka 2015.
Linapokuja suala la upenzi wa vyama, ukweli uko wazi, CCM inaendelea kuwa na wafuasi wengi zaidi kuliko vyama vingine. Wahojiwa walipoulizwa wangependa kumpigia kura mgombea wa chama gani kwenye nafasi za Rais, Mbunge au Diwani, CCM inaongoza kwa mbali. Karibu mara mbili ya idadi ya wahojiwa wanasema watawachagua wagombea wa CCM kwa nafasi hizi, ikilinganishwa na mpinzani wake Chadema. Vile vile 54% ya walioshiriki kwenye utafiti wa Sauti za Wananchi wanasema kuwa wao ni wafuasi wa CCM, wakati wahojiwa 27% walijitambulisha kuwa ni wafuasi wa Chadema.